Friday, October 26, 2012

beki wa kushoto wa klabu ya manchester united patrice evra amewaambia mashabiki kupitia tovuti ya klabu hiyo kuwa umefika muda muafaka sasa kwa man united kudhihirisha ubora wake kutokana na kuwa na michezo muhimu ndani ya wiki kadhaa zijazo evra amesema vita ya kugombea ubingwa wa ligi kuu ya uingereza msimu uliopita ilikuwa ni kwa timu mbili mahasimu kutoka katika jiji la manchester lakini sasa anaamini kuwa msimu huu vita itakuwa kubwa zaidi kwani kuna timu ambazo zimejidhatiti vilivyo kunyakua kombe hilo akizitaja kuwa ni pamoja na chelsea ambayo inaongoza msimamo wa ligi kwa sasa arsenal man city lakini pia hakusita kuitaja na liverpool ambayo bado inasuasua katika msimamo wa ligi kuu ya uingereza

Patrice Evra: Manchester United full-back is ready for an important few weeks

No comments:

Post a Comment