Thursday, October 25, 2012
klabu tajiri ya anzhi makhachakala ya nchini RUSSIA imeibuka na kutangaza nia ya kumsajiri nyota wa manchester united wayne mark rooney mkurugenzi wa benchi la ufundi wa klabu hya anzhi ambaye ni nyota wa zamani wa klabu ya real madrid pamoja na timu ya taifa ya brazil roberto carlos amesema klabu hiyo ina uwezo wa kumsajiri mchezaji yeyote yule nyota duniani kama ilivyofanya kwa samwel eto`o lakini carlos ameongeza kwa kusema rooney ni moja ya wachezaji bora duniani na klabu nyingi za italia pamoja na hispania zimekuwa zikitamani kupata huduma yake lakini sasa anzhi makhachakala italivalia njuga suala hili na kuhakikisha wayne mark rooney anatua katika klabu hiyo mara wakati muafaka wa kufanya jambo hilo utakapofika
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment