Wednesday, October 31, 2012
mchezaji nyota wa fc barcelona lionel andres messi mwenye umri wa miaka 25 ameibuka na kutoa kauli kuwa kura yake ya mchezaji bora wa dunia inaweza kumuangukia xavi hernandez ama andres iniesta lakini pia mchezaji mmoja wa nchi yake messi ametoa kauli hiyo huku akisisitiza kuwa wachezaji wa real madrid wanapaswa pia kupewa kura za kutosha kwani ni wachezaji wenye kiwango cha juu akimtaja golikipa iker casillas na cristiano ronaldo lakini pia messi hakusita kusema lake la moyoni kuhusu uhusiano wake yeye na ronaldo akiongea na gazeti maarufu la habari za michezo nchini hispania maarufu kama marca messi amesema cristiano ni mchezaji wa kiwango cha juu na mara jambo lolote linapotokea magazeti huandika na kuwafananisha nyota hao jambo ambalo kwake yeye amesema linamchosha kiasi ameendelea kwa kusema kuwa vita yao huwa pale wanapokuwa uwanjani na si vinginevyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment