kiungo mkongwe wa manchester united ryan giggs amewashukia na kuwatahadharisha wachezaji wenzake wa klabu ya man united kwamba wanapaswa kujidhatiti na kuwa makini katika mchezo wa jumapili dhidi ya chelsea katika uwanja wa stamford bridge maneno ya giggs yamekuja mara baada ya kuona kikosi cha mashetani wekundu kikisumbuliwa sana na safu ya ulinzi ambayo kwa sasa inaongozwa na mkongwe rio ferdinand pamoja na john evans giggs amesema katika michezo kadhaa ambayo man united imecheza hivi karibuni imekuwa ikitoka nyuma baada ya kufungwa na hatimaye kupata ushindi akitolea mfano mechi ya stoke city pamoja na ile ya ligi ya mabingwa dhidi ya braga lakini akatoa tahadhari kwamba kama hali itakuwa hivyo dhidi ya chelsea basi man united inaweza kupokea matokeo mabaya na ya kushangaza kwan chelsea kwa sasa ni timu ambayo imejengeka upya kwa kuwa na nyota wenye vipaji vya hali ya juu kama eden hazard juan mata pamoja na oscar emboaba da silva juniour
Ryan Giggs warns Manchester United team-mates ahead of Chelsea clash
No comments:
Post a Comment